Serikali imesema imevunja lengo ililojiwekea la kudahili wanafunzi
katika sekta ya afya kutoka wanafunzi elfu kumi kwa mwaka na kufikia
elfu kumi na moja na mia katika mwaka wa masomo 2015/2016 ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa mpango wake wa kulifanya taifa liwe na
watalaamu wa kutosha wa sekta ya afya.
Waziri wa afya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kuongeza kuwa katika bajeti ya safari hii wamedhamiria kuyatua matatizo yote sugu yanayokabili sekta ya afya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za jamii kupitia mwenyekiti wake Peter Serukamba pamoja na kambi rasmi ya upinzani bungeni kupitia msemaji wake Dr.Godwin Mollel wamesema hali ya upatikanaji wa huduma za afya ni mbaya na ni bora Serikali ikaangalie namna ya kuiboresha hasa maeneo ya vijijini.
Baadhi ya wabunge wakichangia bajeti ya wizara hiyo wamesema hospitali kuhudumiwa na wizara mbili tofauti ya afya na Tamisemi kunasababisha huduma kuzidi kulegalega kwa kile kinachoonekana wizara hizo kutegeana.

Post a Comment