Mji mmoja nchini
Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya
pesa. Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la
Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na
uhaba wa pesa nchini humo.
Kituo cha radio kinachofadhiliwa na
Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo
kama aibu kubwa kwa mamlaka.
Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na
hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni,
lakini wanataka pesa zao.
Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni.
Mamlaka
za Uzbekistan hazikubalii uhuru wa vyombo vya habari na raia wa huko
hutegemea vyombo vya habari vya kimataifa kutoa sauti yao, ila
hawajitambulishi.
Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka
sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi
na malipo ya uzeeni.
Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali
katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa
mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.
Post a Comment