Baada ya uongozi wa klabu ya Simba April
20 2016 kutangaza kumfungia mechi tano mchezaji wao Hassan Kessy kwa
sababu za kucheza faulo ambayo ilimpelekea kuoneshwa kadi nyekundu na
kuigharimu timu, usiku wa May 5 2016 mtandao wa salehjembe umeripoti
kuwa beki huyo yupo katika hatua za mwisho kusaini Yanga.
Katika mahojiano na salehjembe Kessy na
meneja wake Hassan Tippo ‘Zizzou’ wamekubali kuwa wamefanya mazungumzo
na Yanga na wapo katika hatua za mwisho kusaini mkataba Ijumaa ya May 6
2016, lakini pia Kessy anadaiwa kuomba apewe jezi namba 25 ambayo
ilikuwa inatumiwa na Emmanuel Okwi wakati yupo Yanga.
Hassan Kessy anaripotiwa kukaribia
kumaliza mkataba ndani ya klabu ya Simba, lakini amefungiwa mechi 5 na
Simba baada ya kumchezea faulo inayodaiwa kuwa ni ya makusudi
Christopher Edward katika mchezo kati ya Simba dhidi ya Toto Africans.
Post a Comment