MKAZI wa kijiji cha Busongola wilayani Mpanda anayedaiwa kuwa jangili
sugu, Harumkiza Joshua (28), ameuawa kwa kupigwa risasi katika
majibizano ya risasi na polisi waliokuwa kwenye msako maalumu wa
wahalifu.
Aidha katika msako huo, Polisi imewakamata wakazi wanne wa kijiji hicho kwa kosa la kumiliki bunduki aina ya SMG namba TX 5971-1996, risasi 86, magazini mbili na nyama inayodhaniwa kuwa ya kiboko kilogramu mbili kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damasi Nyanda, alithibitisha tukio hilo na kuwataja watu hao wanne kuwa ni Amos Maliyatabu, maarufu kama ‘Samandale’ (70) na mwanawe James Amos ‘Samandale’ (28), Leoben Kagoma ‘Karumanzil’ (25) na Kulwa Joseph maarufu kwa jina la ‘Daniel’ (27).
Kamanda Nyanda alisema msako huo ulifanyika hivi karibuni katika kijiji hicho na maeneo mengine ya mkoa mzima. Alisema magazini moja ina uwezo wa kubeba risasi 30 na nyingine risasi 45 kwa wakati mmoja.

Post a Comment