Klabu ya Barcelona
italazimika kushinda mechi zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi
ya La Liga kwa kuwa huenda wapinzani wao wasipoteze hata pointi moja
kulingana na kocha Kuis Enrique.
Viongozi Barcelona walioanza
mwezi wa April wakiwa na pointi nane kileleni mwa ligi hiyo,wako sawa
kwa pointi na Atletico Madrid huku Real Madrid ilio nafasi ya tatu
wakiwa nyuma kwa pointi moja.
''Haiwezekani kwamba timu zilizo nyuma yetu zitapoteza pointi'',alisema Enrique siku ya Ijumaa.
''Mchezo wetu ni mzuri katika kipindi hiki cha mwisho''.
Barcelona iko mbele ya Atletico kutokana na tofauti ya mabao.
Barca,Atletico na Real Madrid zote zinacheza Jumamosi katika muda tofauti.
KIabu ya Zinedine Zidane inaweza kwa masaa machache
kupanda katika kilele cha ligi iwapo itashinda dhidi ya Real Sociedad
katika mechi ya mapema.
Post a Comment