Mei 6 2016 Waziri wa Viwanda, biashara na Uwekezaji Charles Mwijage aliwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Katika hotuba yake, Waziri Mwijage aligusia sekta mbalimbali kama vile Viwanda vidogo na Biashara ndogo, Masoko. ..>>>’Ujenzi
wa uchumi wa viwanda ni vita, tena vita kubwa sana. Mafanikio katika
uchumi wa viwanda yatasababisha nchi yetu kuwa Taifa la watu wa kipato
cha kati‘
‘Katika
mwaka 2016/2017, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya Shilingi
Milioni 20 ikilinganishwa na lengo la Shilingi Milioni 12 na elfu 14 kwa
mwaka 2015/2016 kutokana na ada za leseni, uuzaji wa nyaraka za zabuni,
faini kwa kukiuka Sheria ya leseni na makusanyo mengineyo‘
‘Katika
mwaka 2016/2017, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaomba
kutengewa jumla ya Shilingi 81,871,992,000, ili kutekeleza majukumu ya
Wizara. Ni jukumu kubwa na nyeti ambalo linapaswa kuendelea kuungwa
mkono na wapenda maendeleo wote hasa Watanzania wazalendo‘
Unaweza kuendelea Kumsikiliza hapa chini kwenye hii video….
Post a Comment