0

Mshambuliaji wa Yanga, Matheo Anthony akishangilia bao la pili aliloifungia timu yake katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya GD Sagrada Esperanca uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
 Benchi la ufundi la timu ya Yanga.
Benchi la ufundi la  GD Sagrada Esperanca
 Msuva akimiliki mpira.
 Simon Msuva akimtoka beki wa GD Sagrada Esperanca
 Amissi Tambwe akiwania mpira na mchezaji wa GD Sagrada Esperanca, Manuel Sallo Conho.
 Beki wa Yanga, Kelvin Yondani akimtoka Manuel Paulo Joao.
 Kipa wa GD Sagrada Esperanca, Roadro Juan Da Semero akiokoa mpira.
 Wachezaji wa Yanga wakibadilishana mawao na kocha wao.
 Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo.
 Malimi Busungu akipata matibabu baada ya kuumia uwanjani.
Matheo Anthony akishangilia na Simon Msuva baada ya kuipatia timu yake bao la pili.
 Mei 7 ,2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao mashabiki wao tayari mtaani wanajitamba na kujiita Mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu, wameshuka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili wapinazani wao GD Esperanca katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika. 

Yanga ambao walipangwa na GD Esperanca baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri jumla ya goli 3-2 katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wapinzania wao kutokea Angola klabu ya GD Esperanca, lakini Yanga watalazimika kwenda Angola wiki mbili zijazo kucheza mchezo wa marudiano. 
 
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote na kwenda mapumziko bila kufungana, lakini awali Eperanca walikuwa wanacheza mpira wa taratibu na kujitahidi kumiliki mpira ili kuituliza presha ya mchezo, hali ambayo ilifanya Yanga wabadilke na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 71 kupitia kwa Simon Msuva, kuingia kwa Matheo Anthony kulizaa matunda baada ya dakika ya 90 kufunga goli la pili.

Post a Comment

 
Top