0

                                     

Timu ya likongowele fc imeibuka na ushindi wa goli 4-3 dhidi ya Mnalani fc katika mchezo wa ligi ya Mbuzi Vijana Cup uliopigwa katika uwanja Shule ya Msingi Muungano wilayani Liwale mkoani Lindi.

Magoli  ya timu ya Likongowele yamefungwa na Twaha Tido katika  dakika ya 39,SelemaniMpoto katika dakika ya 47 na 60 huku goli la mwisho likifungwa Faraji Mayai na kwa upande wa Mnalani magoli yao yamefungwa na Imani Mohammedi aliyefuga goli mbili katika dakika ya 15 na 25 na goli la mwisho likifungwa dakika ya 74.

Katika mchezo wa leo mchezaji Abbuu Matwiko wa Likogowele fc na Abdulai ndandala wa Mnalani wameoneshwa kadi nyekundu katka dakika ya 85 baada ya kurushiaa matusi.

Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Mnalani Kasimu Malunga amesema kuwa walizidiwa nguvu na wapinzani wao lakini pia uzembe wa mabeki wake kushidwa kujipanga vizuri umesababisha wao kupoteza mchezo huo na wanajipaga kufanya vizuri katika mchezo ujao.

Pia kocha wa Likongowele Matisho Saidi amesema anamshukuru Mungu kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo na vijana wake wamefuata maelekezo aliyowapa mazoezini.

Post a Comment

 
Top