Serikali mkoani Lindi imewataka watu wote
waliovamia maeneo ya hifadhi ya misitu na
kuendesha shughuli za kilimo kuacha na kuondoka mara moja kabla hawajachukuliwa hatua ya kisheria.
Agizo hilo amelitoa
mkuu wa mkoa wa Lindi Godfray
Zambi kwenye uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kimkoa uliofanyika kijiji
cha Lipuyu wilaya Nachingwea mkoani Lindi
Zambi alisema matumizi ya
misitu na ardhi kwa wananchi ni haki yao ya kimsingi
ambayo inapaswa kulindwa
kwa mujibu wa sheria
lakini ikumbukwe kuwa haki hiyo lazima iambatane na wajibu ili ziweze
kutumika kiuendelevu.
Alisema kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano John Magufuli amejitoa sadaka kwa ajili ya kutetea wananchi kwa
kupambana bila hofu kulinda raslimali
za nchi ili kila mtanzania aweze
kunufaika na raslimali hizo, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kumuunga mkono
kwa kulinda na kuhifadhi rasilimali za nchi kwa bidii , uaminifu na uadilifu mkubwa.
Kwa upande wake afisa maliasili mkoa wa Lindi Zawadi Jilala alisema Mkoa wa lindi una jumla ya hekta 6,785,532
ambazo kati ya hizo hekta 5,238,431 sawa na asilimia 77.2% ya eneo la mkoa
,zimefunikwa na uoto wa asili ambao ni misitu na pori .Mkoa wa Lindi una misitu
ya hifadhi isiyopungua hekta 717,692 ambayo imehifadhiwa na inasimamiwa
kisheria.
Miongoni mwa misitu hiyo ni
kuna misitu ya hifadhi ya Taifa ambayo ina jumla ya hekta 370,304,misitu
ya hifadhi ya Vijiji yenye jumla ya hekta 341,465,Misitu aina ya mikoko ambayo
iko katika mwambao wa bahari ya hindi yenye ukubwa wa hekta 2,723 pamoja na
misitu ya kupandwa ambayo inachukua ukubwa zaidi ya hekta 3000.
Jilala alisema Kwa takwimu ya rasilimali ya misitu ya taifa
iliyotolewa mwezi May ,2015 Mkoa unashika nafasi ya pili katika mikoa yenye
maeneo makubwa ya misitu nchini ikiongozwa na mkoa wa Katavi ambao asilimia
82.7 ya eneo la mkoa limefunikwa na misitu.
Alisema Kutokana na
uwezo mdogo wa taasisi za serikali kifedha na kiutumishi katika kusimamia misitu,mkoa umeamua
kuwapokea na kuwashirikisha wadau
mbalimbali kwenye usimamizi wa misitu
ambao ni ,TFCG,MJUMITA na LIMAS. WWF,MCDI,
Afisa huyo aliongeza kuwa Kupitia mradi wa usimamizi
shirikishi wa misitu (PFM) ambao unawezeshwa na wadau hao ,Juhudi zinafanyika
na kuto elimu katika ngazi zote za vijiji hadi mkoa kuhusu utunzaji shirikishi
wa misitu.
Alisema Baada ya mafunzo hayo serikali itawekeana mikataba
mbalimbali ya kusimamia na kuhifadhi misitu
.Mikataba hiyo itashirikisha wadau mbalimbali na itahusu usimamizi wa
pamoja wa hifadhi za Taifa( JFM) ,Jamii kuwa na misitu yao wenyewe( CBFM) na
watu binafsi kuwa na mistu yao wenyewe mikatab hiyo itazingatia haki ya
matumizi na mgawanyo wa mfano na gharama zitokanazo na misitu husika.
Jilala alisema Jumla ya hekta 341,465 za misitu ya hifadhi ya
vijiji ( Village Land Forest Reserves- VLFR) katika vijiji 85 imeshahifadhiwa na inaendelezwa na
kusimamiwa kikamilifu,pia jumla ya misitu ya vijiji 62 kwa wilaya ya Lindi
,Ruangwa,Kilwa na Nachingwea imeshakabidhiwa rasmi kwa serikali za vijiji na
imesimamiwa na kuendelezwa na wanavijiji weneyewe kwa kushirikiana na wataalam
wa misitu kutoka wilayani.
Alisema misitu 6 ya
hifadhi ya Taifa ,yenye jumla ya hekta 189,417 inasimamiwa kwa usimamizi
wa pamoja( JFM) na jumla ya vijiji 27 , imefikia katika hatua za mwisho ili
iweze kusimamiwa na kuendelezwa na vijiji hivyo kwa kushirikiana na wataalam wa
misitu kutoka wilayani .Kufuatia mafanikio ya program hii kumekuwa na mwamko
mkubwa kwa wanakijiji hasa kwa vijiji vile ambavyo havijfanikiwa na wafadhili
hawa.
Aidha mipango ya kuvifikia vijiji vingine kwenye wilaya zote
unaendelea .Nitarajio na kusudio la serikli kuona kuwa vijiji vilivyotenga
maeneo haya vinanufaika kwa njia ya uvunaji endelevu na uendeshaji na shughuli
zingine rafiki kwa mazingira na hivyo kuchangia katika kupunguza umaskini na
kutekeleza MKUKUTA.
Post a Comment