Wakili Moses Mkapa (kushoto) akipeana mikono na mteja wake Mbunge wa jimbo la Liwale,Zuberi Kuchauka
Kesi ya upingaji matokeo ya ubunge katika jimbo la Liwale mkoani Lindi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa zamani jimbo hilo mwaka 2010-2015 Mh.Faith Mitambo (ccm) baada ya kushindwa kupata kura za kutosha na kushindwa kutetea kiti hicho na kushinda mpizani wake Mh.Zuberi Kuachauka (Cuf) leo imefutwa rasmi na jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo na kumpa ushindi mh.Zuberi Kuchauka baada ya mlalamikaji kushindwa kutokea mahakamani.Aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Liwale mwaka 2010-2015 mh.Faith Mitambo
Mahakama kuu kanda ya kusini
imelitupa mbali Shauri la mgombea ubunge jimbo la Liwale mh. Faith Mitambo la
kupinga matokeo ya ushindi wa
mbunge wa jimbo hilo Zuberi Kuchauka (CUF)
shauri hilo
Namba 2 la mwaka 2015, pamoja na mambo mengine Mitambo alikuwa akipinga ushindi
wa Kuchauka (CUF) akidai kuwa taratibu kadhaa cha uchaguzi zilikiukwa.
Mitambo
alilalamika kuwa kuna baadhi ya
taratibu zilikiukwa akidai kuwa
Kuchauka alifanya kampeni siku ya
uchaguzi na kwenye baadhi ya vituo vya
kupigia kura idadi ya wapiga kura ilikuwa kubwa kuliko waliojiandikisha
Akisoma
hukumu ya shauri hilo jana, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Rehema .K Mkuye,
alisema ametupilia mbali kesi hiyo baada ya mlalamikaji pamoja na wakili wake
kushindwa kufika mahakamani katika muda uliopangwa bila kutoa taarifa yoyote.
Jaji Mkuye
alisema kwa mujibu wa kanuni ya 27 (1) ya kanuni ya sheria ya uchaguzi GN namba
447 ya mwaka 2010, inasema wazi kuwa endapo mlalamikaji katika mashauri ya aina
hiyo atashindwa kufika mahakamani bila taarifa, kesi yake huwa inaondolewa
mahakamani.
Alisema
pamoja na kuiondoa kesi hiyo mahakamani, mlalamikaji atakazimika kulipa gharama
za shauri hiyo ya kupinga matokeo.
Mapema
Wakili wa Serikali, Peter Maugo aliiomba mahakama kulitupilia mbali shauri hiyo
kutokana na upande wa mlalamikaji kushindwa kufika mahakamani hapo kama
ilivyopangwa.
Katika
sheuri hilo, Wakili Maugo alishirikiana na wakili mwingine wa serikali Charles
Mtaye ambapo pamoja waliungana kumuomba Jaji Mkuye kulitupilia mbali shauri
hili kwa sababu limekosa mashiko.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kesi hiyo kuamriwa, Wakili wa Kujitegemea wa upande
ulioshinda (mlalamikiwa), Moses Mkapa alisema shauri lilikwenda vizuri na
kwamba matokeo ya ushindi kwa mteja wake umempa faraja.
"Kesi
imekuwa na mwenendo mzuri na kabla ya uamuzi wa leo (jana), pande zote husika
zilikubaliana mahakamani hapo Aprili 12 kwamba shauri lingeanza kusikilizwa
jana kuanzia saa 2:00 asubuhi, lakini hadi kufikia saa 4:45 upande wa
mlalamikiwa hakukuwa na mtu hata mmoja mahakamani," alisema Mkapa.
Kwa upande
wake mbunge mlalamikiwa Zuberi kuchauka ,alisema kuwa
haki imetendeka na ana mshukuru mungu
kwa ushindi aliopata na kwamba mahakama imetenda haki yake.
Post a Comment