0

Zaidi ya wafanyakazi mia moja wa mgodi wa uchimbaji wa  madini ya Tanzanite ya G and M uliyopo katika Mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameandamana kupinga hatua ya kampuni hiyo kuwaachisha kazi bila kuwapa stahiki zao kwa kazi waliofanya kwa zaidi ya miaka mitatu huku wakilazimishwa kusaini mikataba mipya.
Wakizungumza kwa jazba wafanyakazi hao wamesema wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka mitatu na sasa wameachishwa ghafla kwani walifika kwenye lango kuu la kuingia mgodini wamekuta pamefungwa na kutakiwa wasiingie ndani,wameiomba serikali iwasaidie kwakuwa tayari wamiliki wameajiri wafanyakazi wengine na wao kulazimishwa kusaini mikataba mipya.
 
Mwenyekiti wa wafanyakazi hao  Adam Mosha amesema hatua iliyo chukuliwa na uongozi wa mgodi huo siyo ya kibinadamu na kamwe hawatakubali kuacha haki yao.
 
ITV ilimtafuta Meneja wa Mgodi huo Elisante Forcet ambaye amedai kuwa  kampuni hiyo haijawahi kuajiri wafanyakazi lakini huwa wanawachukua kama vibarua na hivyo hakuna mwenye haki ya kudai na kwa sasa kampuni haina pesa za kuendelea kuwa na wafanyakazi wengi kiasi hicho.

Post a Comment

 
Top