0
YangaKikosi cha Yanga
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm, amesema atahakikisha wanafanya maandalizi mazuri kuweza kuikabili timu ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Raundi ya Pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika .
Yanga imefuzu hatua hiyo baada ya kuitoa APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2 kwa mechi mbili wakati Al Ahly iliibwaga Libolo ya Angola jumla ya Bao 2-0 baada kutoka Sare 0-0 huko Angola kufuatia ushindi wa bao 2-0 mjini Alexandria.
Mara ya mwisho kwa Yanga na Al Ahly kukutana katika michuano hii ilikuwa msimu wa 2013/14 ambapo Yanga walishinda 1-0 mjini Dar es Salaam na Al Ahly kushinda 1-0 huko Misri na Al Ahly kusonga mbele baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Pluijm amesema kuwa anaijua Al Ahly ni timu ngumu na inabidi wajipange ili waitupe nje.
Yanga na Al Ahly zitakutana Aprili 8-10 mjini Cairo, Misri kwa mechi ya mkondo wa kwanza, na mechi ya marudiano itachezwa Aprili 19-20 Dar es salaam.

Post a Comment

 
Top