0
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne wa huduma za Misitu na wanyama Pori.

           
Mkurugenzi Wanyamapori atumbuliwa kwa kutoa vibali kusafirishia Tumbili 61 kwenda Albania
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyamapori Dkt.Charles Mulokozi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kuhusika kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili 61 kupitia uwanja wa ndege wa kimatifa ya Kilimanjaro-KIA- kwenda Albania kinyume cha  taratibu.
Uamuzi huo wa Profesa.Jumanne Maghembe umetokana na jeshi la Polisi kukamata rai wa wawili wa Uholanzi katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa katika ndege ya kukodi ya Afrika Kusini wakiwa na Tumbili 61 wakijaribu kuwasafirisha kuelekea nchini Alabinia huku zaidi ya Tumbili 450 wakiwa wamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali nchini wakiwa katika mpango wa kusafirishwa kuelekea nchini humo.
 
Aidha Profesa.Maghembe amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi viongozi waandamizi sita akiwemo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania Bwana. Juma Mgoo,Mkurugenzi wa  rasilimali Misitu Bi.Zawadi Mbwambo,Mkurugenzi wa matumizi ya rasilimali misitu pamoja na  Mkurugenzi wa biashara na huduma Bwana Emmanuel Wilfred pamoja na baadhi ya mameneja wa kanda kutokana na kukamatwa magogo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 wilayani Karambo Yakiwa katika mpango wa kusafirishwa kwenda nchni china.

Post a Comment

 
Top