Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya
miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart
Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto)
kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa
njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji
cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja
Kadogosa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia)
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement),
Bw. Reinhart Swart (kushoto) wakisaini makubaliano ya kusafirisha saruji
ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma
na Mwanza. Huku Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wakishuhudia.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL)
Bw. Masanja Kadogosa (kulia) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha
saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya
Kigoma na Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji
cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji
cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja
Kadogosa
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua
jambo baada ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda
hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba
Cement), Bw. Reinhart Swart na (Kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw.
Martine Shigela.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga
(Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) wakipakia mfuko wa
saruji kwenye kontena kabla ya kuanza kusafirishwa kwa njia ya reli
kutoka katika kiwanda cha Simba Cement kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
………………………………………………………………………………………………….
Kiwanda
cha Saruji Tanga (Simba Cement), kimeingia makubaliano na Shirika la
Reli Tanzania (TRL), kusafirisha shehena ya saruji kwa njia ya reli
kutoka mkoani Tanga kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Chini
ya Makubaliano hayo zaidi ya tani laki nne na nusu zitasafirishwa kwa
mwaka na hivyo kupunguza gharama ya bei ya Saruji katika mikoa ya Kanda
ya Ziwa na Magharibi kutokana na usafirishaji wa reli kuwa wa bei nafuu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema katika
mkataba huo TRL litapata zaidi ya shilingi Bilioni 40 na hivyo kufufua
huduma ya usafirishaji wa mizigo katika reli ya kati na kuongeza mapato
kwa nchi.
Prof.
Mbarawa amewataka wafanyabiashara nchini kuanza kutumia reli
kusafirisha bidhaa zao, kwani usafiri huo ni salama na nafuu na
unachukua shehena kubwa kwa wakati mmoja.
“Asilimia
95 ya mizigo hapa nchini inasafirishwa kwa barabara hivyo mkakati wa
Serikali wa kufufua viwanda utafanikiwa kwa haraka endapo wasafirishaji
watatumia njia ya reli “, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha,
amefafanua kuwa usafirishaji wa reli ukiimarika utapunguza ajali za
barabarani zinazosababishwa na malori na kupunguza kasi ya uharibifu wa
barabara unaotokea sasa kutokana na maroli kuzidisha uzito.
Prof.
Mbarawa amewataka watumishi wa TRL na wananchi kulinda miundombinu ya
reli na kutumia fursa ya usafiri huo kujiongezea mapato.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela amesema usafirishaji wa
mizigo kwa njia ya reli utatoa fursa za ajira na kuwezesha bandari ya
Tanga kupata shehena kubwa ya mizigo na hivyo kurudisha hadhi ya Mkoa wa
Tanga.
“Tanga
tuna reli, barabara na bandari hivyo tukio la kuanza kusafirisha mizigo
kwa njia ya reli itaongeza shehena kubwa katika bandari ,itatengeneza
ajira kwa wakazi wa Tanga na kukuza uchumi wa mkoa”, amesema Bw.
Shigela.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRL) Bw. Masanja
Kadogosa amesema kusainiwa kwa mkataba huo kutawezesha TRL kusafirisha
tani elfu thelathini na tano za Saruji kati ya tani laki moja na elfu
tano zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji Tanga Bw. Reinhart Swart, amesema
usafirishaji wa Saruji kwa njia ya reli utaongeza kasi ya usafirishaji
wa saruji na kuwezesha kuwafikia watumiaji kwa bei nafuu.
Kiwanda
cha Saruji Tanga kinakuwa kiwanda cha kwanza kuingia mkataba na TRL
kusafirisha shehena ya mizigo tangu Serikali kuanza mikakati yake ya
kufufua reli na kupunguza usafirishaji wa shehena kubwa kwa njia ya
barabara na hivyo kuzuia uharibifu wa barabara na kupunguza ajali.
Post a Comment