0

Biashara za utalii visiwani Zanzibar zimedorora kutokana na hofu kwa wafanyabiashara za utalii, shughuli za utalii, uongozaji wa watalii pamoja na Hoteli za kitalii kufungwa kwa muda.

Hofu hiyo imeelezewa na wafanya shughuli hizo kuwa ni kutokanana hali ya kisiasa visiwani humo ambayo ilizua uoga kutokana na habari za kuiwepo kwa tishio la amani.

Katika maeneo ya Stone Town Unguja, Forodhani pamoja na maeneo mengine ya utalii hali ya ukimya ilitawala siku kadhaa ambapo wafanyabiashara za utalii wameiambia East Africa Radio kuwa hali hiyo iliwaathiri sana kimapato.

Ibrahim Jabir anafanya kazi ya kusafirisha watalii kwenda katika visiwa vidogo vidogo vya Changua kutoka Mji Mkongwe Unguja Zanzibar na yeye ameeleza athari hiyo ilivyowakabili na kusema kuwa wanaiomba serikali kurejesha hali kwa kutoa taarifa chanya za hali ya kiusalama ili kurejesha biashara na hali ya kiuchumi.

Post a Comment

Top