0

  Michuano ya Kombe la Shirikisho nchini FA katika hatua ya Robo fainali inatarajiwa kuendelea alhamisi ya Machi 31 kwa kupigwa michezo miwili.
Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, mchezo mmoja utawakutanisha Azam FC wakicheza dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons Uwanja wa Chamazi huku Yanga SC wakishuka dimba la Uwanja wa Taifa kuwakaribisha Ndanda FC.
 

Kizuguto amesema, hatua ya robo fainali itahitimishwa Aprili 11 mwaka huu kwa wekundu wa Msimbazi Simba SC kuwakaribisha Coastal Union Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mpaka sasa ni timu ya Mwadui FC pekee iliyofuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Geita Gold bao 3-0 mwishoni mwa wiki ambapo anasubiri timu tatu kuungana nazo kwa ajili ya hatua ya nusu fainali itakayochezwa mwishoni mwa wiki ya mwisho ya mwezi wa nne ambapo bingwa wa mwaka huu ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Post a Comment

 
Top