Mtu
mmoja mkazi wa Mbangala – Chapwa wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina
la Erasto Vickson [17] alifariki Dunia baada ya gari yenye namba za
usajili T.806 ABY aina ya mitsubishi Fuso lori lililokuwa likiendeshwa
na dereva aitwaye Masoud Wilson Nzowa kushindwa kupanda mlima na kisha
kurudi nyuma.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 15.03.2016 majira ya saa 09:45 asubuhi huko
mtaa wa Chapwa, kata na tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa
Mbeya.
Inadaiwa
kuwa, marehemu ambaye alikuwa abiria kwenye gari hilo aliruka toka
ndani ya gari baada ya kuona gari limeshindwa kupanda mlima na kuanza
kurudi nyuma. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kituo cha afya Tunduma.
Dereva alikimbia baada ya tukio. Upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na
kumtafuta mtuhumiwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z.
Msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa
wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za
kisheria.
Imesainiwa na:
[Ahmed Z. Msangi – SACP]
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.
Post a Comment