MAOFISA WA MISITU MKOA WA LINDI WATAHADHARISHWA DHIDI YA UHARIBIFU MKUBWA WA MISITU
TANGAZO
Baadhi ya Vipande Vya mbao vilivyokamatwa na maofisa misitu (Picha ya Maktaba)
Christopher Lilai,Nachingwea.
Mkuu mpya wa mkoa wa
Lindi,Godfrey Zambi amewatahadharisha maafisa misitu ambao wilaya zao zitakuwa
na uharibifu mkubwa wa misitu mkoani humo kuwa watakuwa ndio wa
kwanza kuchukuliwa hatua kali kwa kushindwa kusimamia misitu.
Akihutubia wananchi wa
kijiji cha Lipuyu, wilayani Nachingwea, mkoani Lindi wakati wa siku ya upandaji
miti kimkoa iliyofanyika katika kijijini hapo siku ya jumanne, ambapo pia
alizindua mradi wa maji katika kijiji hicho alisema haiwezekani uharibifu mkubwa
wa misitu uendelee kuwepo wakati wapo wanaotakiwa kusimamia kwa kudhibiti
vitendo hivyo.
Alisema kuwa baadhi ya
maafisa misitu ndio chanzo kikubwa cha ukataji miti ovyo kwani ndio wanaoruhusu
mazao ya misitu kusafirishwa bila ya kuzingatia taratibu na sheria
zinazosimamia misitu.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa
ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli aliwataka wananchi mkoani
hapa kutofanya shughuli za kibinadamu zinazoathiri misitu hasa kilimo cha ufuta
kwani madhara ya ukataji wa miti hayawezi kuonekana kwa haraka
bali vizazi vijavyo ndio watakaopata athari zaidi.
“Kama wazee wetu
wangemaliza misitu yote leo hii hali ingekuwaje na kama kilimo yapo maeneo
ambayo yameruhusiwa kwa shughuli za kibinadamu hivyo wananchi wafuate taratibu
za zilizowekwa katika maeneo yao”alisema Zambi.
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa mkoa ambaye aliyefanya ziara yake ya kwanza mara baada
ya kuapishwa wiki iliyopita aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi
watendaji mkoani Lindi kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa
mara kwa mara kuhakikisha kuwa idadi ya miti inayopandwa kila mwaka inafikia
milioni moja na nusu kama lengo lililowekwa kitaifa na pia kama bado inaendelea kutunzwa.
Alisema haiwezekani kila
mwaka kumekuwa na siku ya upandaji miti lakini hakuna anayehakiki kama idadi
inayopandwa inafikia au miti hiyo inaendeleaje kutunzwa hadi sasa.
Aliwataka viongozi hao
kuwa na ratiba ya kufanya ukaguzi wa maeneo yaliyopandwa miti wiki mbili kabla
ya siku ya upandaji wa miti kwenye maeneo yao ili kujiridhisha kama miti
iliyopandwa mwaka uliopita kama ipo kuliko kupanda miti kila mwaka huku
inayopandwa haitunzwi.
“Haiwezekani kila mwaka inapandwa miti lakini hatuna uhakika kama inaendelea kuwapo na tena kila mwaka idadi miti inayopandwa inatakiwa kuwa milioni moja na nusu je inafikia idadi hiyo”alihoji Zambi.
Post a Comment