0

 katibu wa chama cha chema wilaya ya Liwale mkoani Lindi Bw. Zidadu Matila (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula kwa katibu  wa timu ya Mikukuyumbu World soccer Bw.Amanzi Ngunduli juzi,timu hiyo ndio ambayo iliweza kufuzu  kuendelea na Ligi ya mkoa daraja ya tatu  katika kituo cha c:Liwale.

Matila akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mbunge viti maalum wa chadema kanda ya Kusini Mh.Lathifah Kigwalilo alibaini vitu alivyokabidhi vilikuwa na thamani ya Shilingi laki nne na elfu moja (401,000/=).

Katibu wa mikukuyumbu Bw.Amanzi Ngunduli alisema anashukuru sana kwa msaada walioupata na anawaomba wadau wengine wajitokeze ili kuweza kusaidia timu hiyo kwani ndio timu pekee kutoka Liwale iliyofuzo kuendelea na mashindano hayo yanayofanyika sasa katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.


Post a Comment

 
Top