March 14 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea Hekaheka iliyotokea Tanga hii ni baada ya ndugu kuchanganya Maiti katika Hospitali ya Bombo, Tanga,
wakwanza kuchukua mwili wa marehemu walishamfanyia taratibu za mazishi
na kuzika, ndipo badae walipo lazimika kufukua mwili baada ya kugundua
siyo ndugu yao.
‘Maeneo
ya Mikanjuni kulitoke msiba wa mzee aliyefahamika kwa jina la mzee
Mhina ndipo walipompeleka kumuifadhi katika Hospitali ya Bombo, na kesho
yake saa nne tulienda kuchukua maiti yetu kwa ajili ya kwenda kuzika
tulifanikiwa kuzika lakini badae uongozi wa Bombo ulifika na kutuambia
ile maiti sio yetu‘>>> Mkazi
‘Aliyeenda
kuchukua mwili wa marehemu Hospitali ni Baba Mdogo, kuuosha pia
alisismamia yeye baba mdogo na walivyorudi nyumbani baba mdogo alikata
watoto wasione maiti ya baba yao mwisho wa siku ili bidi tufukue tuwape
mwili wao na sisi tuchukue mwili wetu‘>>>Shuhuda
Post a Comment