0
NA Mwandae Mchungulike,Liwale
Mbunge viti maalum wa Chadema mh,Lathifa Kigwalilo Jana februari 27,mwaka 2016  alitembelea gereza la Kilimo Kipule lililopo katika kijiji cha Kipule Mangilikiti wilayni Liwale Mkoa wa Lindi ambako alipata nafasi ya kuzungumza na wafungwa na kuwapatia msaada wa vitu kama sabuni,miswaki pamoja na dawa za meno ambazo huduma hiyo walikuwa wamekosa kwa muda mrefu sasa.

Katika ziara hiyo alizikuta Changamoto nyingi sana baadhi ikiwa ni;ukosefu wa Maji safi na Salama hakuna hali ambayo inaweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa ya mlipukoUmeme hakuna katika eneo la wafungwa,umeme wa rea umeishia nje ya magereza katika nyumba za askari magereza Mesi ya chakula imeezekwa na makuti Vyoo vichache na sio vya viwango kabisa,uzio Ukuta wa miti,Wafungwa hawana ndala,Chawa na kunguni kutokana na kukosa dawa za fumigation kwa wakati.


 Upande wa kushoto bwana Zidadu Matila katibu wa Chadema wa wilaya ya Liwale na kulia mh.Lathifa Kigwalilo mbunge viti maalum akitoa msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi
 Mbunge akiwafaraji wagonjwa jana katika ziara yake alipotembelea katika hospitali ya wilaya ya Liwale

Pia katika ziara yake alitembelea katika hospitali ya wilaya ya Liwale iliyopo Mkoa wa Lindi alipowatembelea wagonjwa ambako alitoa msaada wa chandarua katika wodi ya wazazi na alipata fursa ya kuzungumza na kila mgonjwa kwa kuwafariji.


 Mbunge akitoa maelezo kwenye ujenzi wa umwagiliaji ambao ujenzi wake haujakamilika

Akiwa katika kijiji chaMtango kata ya Mbaya wilaya ya Liwale Mkoa wa Lindi ambako alikagua ujenzi wa nyumba ya wauguzi ambayo hadi ilipoanza kujenga kwa kipindi kirefu hadi sasa bado ujenzi wake haujakamilika.

Wananchi wanalazimika kuchangishana kulipia kodi ya wauguzi Pia na mradi wa umwagiliaji ambao ujenzi wake pia haujamalizika hadi leo na haujajengwa katika kiwangoalisema Kigwalilo
 Mbunge viti maalum akikabidhi msaada wa jezi na mipira kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale ambapo jana kulikuwa na ufunguzi wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa katika kituo cha Liwale
 Mbunge viti maalum akikabidhi msaada wa jezi na mipira kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale ambapo jana kulikuwa na ufunguzi wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa katika kituo cha Liwale
 Mbunge viti maalum akikabidhi msaada wa jezi na mipira kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale ambapo jana kulikuwa na ufunguzi wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa katika kituo cha Liwale


Mbunge ameweza kuchangia kuhodhi kituo cha michezo kilichopo katika wilaya ya Liwale kwa kukiwezesha kituo hicho kuendesha ligi ya daraja la tatu ngazi ya mkoa jana kwenye  ufunguzi wa mashindano hayo aliwapatia kila timu jezi na mipira kwa timu tatu za Liwale zinazoshiriki mashindano ya ligi hilo.

Post a Comment

 
Top