0


Siku zote katika maisha ya mwanadamu changamoto au matatizo ni kitu ambacho hakikwepeki. Kila mara binadamu huyu huweza kukutana na changamoto au matatizo haya kwa njia mbalimbali. Wapo ambao wanapokutana na changamoto huweza kuzikabili kirahisi na wapo ambao hukwama kabisa.

Najua na pia naamini kabisa kwa namna yoyote ile umeshawahi kukutana na matatizo katika maisha yako tena hata bila ubishi hata kidogo. Hakuna mtu ambaye hajawahi kukutana na tatizo au changamoto. Kitu cha kujiuliza ulipokutana na tatizo hilo ulifanyaje? Ulikata tamaa au ulisonga mbele?Ni kitu gani ambacho ulifanya?

Katika siku ya leo tutaangalia njia rahisi ambazo unaweza ukazitumia kukabiliana na matatizo hasa pale unapokutana nayo. Njia hizi zitakusaidia sana uweze kutambua kuwa unaweza kufanikiwa hata kama una matatizo. Na pia utaelewa kuwa na matatizo siyo mwisho wa mafanikio. Sasa twende pamoja kujifunza.

1. Amini kila tatizo lina njia ya kutokea.
Inawezekana unaona tatizo ulilonalo ni kubwa sana kiasi cha kwamba halina dawa, lakini si kweli kila kitu kina mwisho wake, ikiwa pamoja na tatizo lako hilo. Kama lilivyoanza ndivyo hivyo litakavyoisha kitu cha kuzingatia kuwa mvumilivu, ingawa maumivu kweli yapo.

2. Tuliza akili yako.
Wakati unatafuta suluhisho la tatizo lako jitahidi sana kutuliza akili yako. Mara nyingi akili huwa haifanya kazi vizuri sana kama upo kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Hivyo ili uweze kupata majibu sahihi ya kile unachokitaka ni vyema ukaituliza akili yako ili ikupe majibu sahihi.
SOMA; Kanuni Sita (6) Muhimu Za Kushinda Tatizo Lolote Ulilonalo.

3. Acha kutafuta majibu ya kulazimisha.
Kwa vyovyote vile tatizo ulilonalo najua lina kukera na hutaki kabisa kuendelea nalo. Sasa hapa unatakiwa kuwa mwangalifu na kitu kimoja, tafuta majibu sahihi. Acha kulazimisha majibu ambayo yanaweza yasiwe msaada kwako. tumia akili yako vizuri kupata majibu ya kweli.

4. Andika kila njia unayoona inaweza kutatua tatizo lako.
Najua unaweza ukawa una majibu kichwani unayoamini yanaweza yakakusaidia. Sasa hayo majibu unayoyaamini yanaweza kutatua tatizo lako yaandike. Yafanye majibu hayo yawe wazi ikiwezekana yaweke sehemu ya wazi, ili yaumbike vizuri kichawani mwako na kukupa majibu halisi.

5.  Jiamini.
Itakuwa ni kazi bure unatafuta namna ya kutatu tatizo lako wakati huo huo hujiamini. Ni vizuri ukajiamini wewe mwenyewe kwanza na ukajua un uwezo wa kulitatua taizo hilo. Bila ya kujiamini itakuawa ngumu kulitatua tataizo lako na litachukua muda mrefu.

6. Tafuta msaada.
Hilo tatizo ulilonalo sio wewe wa kwanza kulipata. Kama ni hivyo basi tafuta msaada kwa watu wengine ambao walishawahi kupitia hali kama yako. Huwezi hiyo soma vitabu vinavyoweza kukusaidia kuhusiana na tatizo lako. Vinginevyo ukibaki peke yako itakuwa ni ngumu sana kuweza kulitatua kiurahisi.

7. Fanya tahajudi (Sala)
Katika kipindi ambacho upo kwenye maatatizo ni vyema ukajijengea utaratibu wa kufanya tahajudi au sala. Hiyo itakusaidia sana kuituliza akili yako na pengine hata kukupa majibu unayotaka moja kwa moja. Sala pia au tahajudi ina nguvu kubwa sana katika akutatua tatizo ulilonalo.

Kwa kufuata hatua hizo, kwa namna moja au nyingine zitakusaidia kuweza kukabiliana na tatizo ulilonalo. Kitu cha muhimu kwako ni kuweza kuchukua hatua na kusonga mbele.

Post a Comment

 
Top