Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi.
Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza kuitoa.Baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuanza kulihutubia bunge baadhi ya Wabunge walianza kupiga filimbi na zikasababisha kelele nyingi mpaka Spika kulazimika kumuomba Rais asiendelee mpaka awatoe kwanza Wabunge hao saba akiwemo mbunge wa Ungunja Opiyo Wanday.
Picha zote kutoka CITIZEN TV Kenya.
Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi.
Hata hivyo utulivu ulirejea baada ya spika kuwatupa nje wabunge waliokua wakizipuliza hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba yake kwa taifa.
Post a Comment