0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Musa Juma Assad amesema bado kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha ndani ya ofice yake ambazo zingewawezesha watumishi wa idara hiyo kutekeleza majukumu yao na kuwafikia walengwa kayika suala zima la ukaguzi wa fedha ndani ya Halmashauri mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye mahojiano na East Africa Radio baada ya kuhudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ambapo ameiomba serikali kuitazama kwa jicho la kipekee ofisi yake ili ifanikishe kazi zake za kiukaguzi.

Amesema kazi ya Ofisi yake ni kuhakikisha Bunge linafanya kazi zake jinsi inavyotakiwa na kuhakikisha inaongeza mahusiano na ofisi nyingine ili kuwe na urahisi wa kufanya kazi pindi inapobidi kufanya kazi hizo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati wa Hesabu za Serikali Mheshimiwa Aeshi Hilaly ameiomba Ofisi ya CAG kutoa ushirikiano kwa Wabunge wa kamati hiyo kwa uwazi na ukweli ili Watanzania wajue matumizi ya Fedha zao.

Post a Comment

Top