Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya
Mkoa wa Pwani-Tumbi kuanza kutumia jokofu moja lenye uwezo wa kuchukua
miili nane (8) katika chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) ya Hospitali
hiyo baada ya kuridhishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kutembelea kwa
mara ya pili kuikagua, tokea alipoipa masaa 72 ifungwe na ifanyiwe
matengenezo.
Dk.
Kigwangalla alifika hospitaalini hapo majira ya saa nane mchana na kisha
kwenda moja kwa moja kwenye jingo hilo la Mochwari na kukuta mafundi
wakiendelea na matengenezo kwa upande wa majokofu ambayo yalikuwa
hayafanyi kazi na kusababisha matatizo hata Naibu Waziri kuagizwa
kufungwa ma siku tatu ili uongozi huo ufanyie matengenezo.
“Nilitoa
masaa 72, muwe mumefanyia kazi tatizo hili. Na leo hii nimerudi tena
kukagua kuona utekelezaji wa agizo langu kama mumelifanyia kazi. Hivyo
kwa kuwa tayari ili jokofu moja limeanza kutengamaa nalifungulia lianze
kazi mara moja na la pili lianze kazi pia litakapokamilika mutujulishe
haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo kwa
uongozi wa Hospitali hiyo ya Tumbi.
Ziara hiyo katika kukagua utekelezaji wa Mochwari hiyo ya Tumbi,
ameifanya jana Machi 13.2016 akiambatana na maafisa wa Wizara yake hiyo
ambapo pia alipata kutembelea Hospitali nyingine ya Jijini Dar es Salaam
ya Sanitas ambayo imefungiwa kutoa huduma kwa upande wa chumba cha
Upasuaji kutokana na kutokidhi vigezo.
Hata hivyo kwa upande wa Hospitali Dk. Kigwangalla alieleza bayana
kuwa, alipata taarifa juu ya uongozi wa Hospitali hiyo kuendelea na
huduma za upasuaji lakini hakukuta hali hiyo na kuendelea kusisitiza
huduma hiyo isifunguliwe mpaka hapo watakapokamilisha vigezo vya Wizara
juu ya Chumba chaa upasuaji kinavyotakiwa kiwe.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog.
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiangalia namna utengenezaji huo unavyoendelea kwa upande wa nje wa majokofu hayo.
Mtaalam wa upande wa Mochwari hiyo ya Tumbi akitafakari jambo wakati wa ujio huo wa Naibu Waziri Dk. kigwangalla.
Post a Comment