0
Simba aliyeuawa katika kijiji cha Namihu kilichopo katika kata ya Mbaya wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.(Picha simba aliyeuawa mara ya kwanza kijijini hapo)
Habari iliyotufikia hivi punde Simba mwingine auawa katika kijiji cha Namihu wilayani Liwale mkoani kuawa kwa simba huyu wa pili ni jitihada za askari maliasili kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho.

Juma liliopita kikundi cha simba kilivamia katika kijiji cha Namihu na kupelekea wakazi hao kusimamisha shughuli mbalimbali kiziwemo za kilimo.

Mtendaji wa kijiji cha Namihu Bw.Amidu Mwembe alisema simba ameuawa leo majira ya saa 5 asubuhi baada ya askari maliasili kwa kushirikiana na wananchi kufanya msako mkali wa siku tatu.



     KUANGALIA PICHA SIMBA ZA SIMBA WA KWANZA ALIYEUAWA BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top