Simba akiwa ameuwawa leo na kuletwa kijijini katika ofisi ya kijiji cha Namihu kilichopo kata ya Mbaya wilayani Liwale mkoani Lindi
Wananchi wa kijiji cha Namihu na vijiji jirani waliofika katika kijiji hicho kumwangalia simba aliyeuwawa

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Namihu wanashindwa kuhudhulia masoma baada ya kijiji hicho kuvamiwa na Simba na kandokando ya shule kuna zizi la kuku walivamia simba na kuweza kula 10 wa bwana Salehe Kapunju.
Na Mwandae Mchungulike,Anna Millanzi na Briligita Kambona,Liwale

Wakazi wa kijiji cha
namihu wilayani Liwale mkoani Lindi wakumbwa na Taharuki mara baada ya kijiji
chao kuvamiwa na simba.
Akizungumza na wandishi
wa habari mtendaji wa kijiji hicho leo bwana Amidu Mwembe amesema ni takriban siku sita sasa
tokea simba hao wavamie katika kijiji hicho .
Aidha mtendaji huyo alisema
taarifa ya kuwepo kwa wanyama hao katika kijiji cha Namihu alizifikisha mapema
wilayani lakini askari hao walifika baada ya siku ya tatu ndipo walipofanikiwa
kumuua simba mmoja huku wengine wakikimbilia katika maeneo ya msituni kijijini hapo.
Kwa upande wa
waathirika wa kijiji hicho bwana Haji Mchunga na Salehe Kapunju walisema simba hao wamefanya uharibifu kwa
kula mifugo yao ya kuku jumla ya 30 na
wameomba msaada wa kuwawezesha kwakuwa mifugo yao ilikuwa ndio tegemeo lao pia wakiilaumu
serikali kwa kuwanyang’anya wananchi waishio jirani na mbuga siraha ambazo
zingeweza kuwalinda na wanyama wakali kama hao.
Huku Salima Kijoga akiongea
kwa niaba ya kinamama alisema wanashindwa kutekeleza majukumu yao kama vile kwenda
shamba kulinda mazao yao yanayoliwa na wanyama waharibifu.
“Katika kata ya Mbaya
kuna tatizo kubwa la chakula kutokana na tatizo la Simba na wanafunzi
wanashindwa kwenda shuleni na leo wakithamini sana wanyama kuliko binadamu sio
vizuri kwani sisi binadamu tunathamani kuliko wanyama”alisema Salima.
Kwa upande wake Mwalimu
mkuu msaidizi wa shule ya msingi Namihu Emanueli Mdidi alisema hata idadi ya
mahudhulio ya wanafunzi imepungua kwa kushindwa kufika shuleni kwa kuhofia
wanyama hao.
Diwani wa kata ya Mbaya bwana Ali Kioi amekili tatizo la kuchelewa kwa askari wa wanyamapori ni ukosefu wa usafiri na
aliongeza kusema tatizo la kuvamia wanyama katika kijiji cha Namihu halijawahi
kutokea takribani miaka 15.

Post a Comment