Waziri
mkuu Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh.
milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye
vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa vijijini
mkoa wa Iringa.
Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko
ambayo yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha
Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda
kukagua athari za mafuriko na kuwapa pole wananchi hao leo mchana
(Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote
waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya
saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita
250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-.
Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya
saruji 200 vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-.
Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa
mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-;
Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na
mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa
tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150,
mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za maharage, kilo 50 za chumvi na nguo
mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-.
Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti
Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM
Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa
Iringa, Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh.
milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni
mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni
20/- kati ya hizo sh. milioni 15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bw. George Simbachawene. Pia
alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa
ni mchango kutoka Benki ya CRDB.
Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati
mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh.
milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la
kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko
hayo.
Mapema, akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Bi. Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi
kutokana na mvua zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla
ya hapo, kaya nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua
zilizoanza Februari 3, mwaka huu.
Alisema miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya
na kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao
walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika
na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao.
“Tangu Februari mosi, wamekkkwishapokea waginjwa wa kipindupinda
351 llakini walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu
huyo wa mkoa.
BODI
ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi
Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha
uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba
amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na
kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo
ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.
“Kumekuwa
na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni
hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa
stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo
wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.
Aidha
Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo
na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji
mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.
Hatua
hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape
Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo
ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21
kuacha kazi.
“Nataka
Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue
hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua
mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.
Hata
hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha
utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji
wa magazeti kwa kiwango kikubwa.
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2016/02/mhariri-mtendaji-wa-magazeti-ya.html#sthash.3ou4RS5O.MvHxj9Qg.dpuf

Post a Comment