Na.Ahmad Mmow, Lindi-Nachingwea.
Ununuzi
wa gari lenye namba usajili DFPA 1695, Landcruiser mali ya Halmashauri
ya Wilaya ya Nachingwea, mwanzo mwa wiki iliyopita ilizua
mvutano baina ya madiwani na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,
Mhandisi, Jackson Masaka.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa pili cha baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha
2015/2016 Madiwani hao walisema walikuwa na mashaka katika ununuzi wa
gari hiyo, kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya fedha zilizotumika
kununulia gari hiyo na bila kuwashirikisha.
Diwani
wa kata ya Mkutokuyana, Sada Makota, alisema mchakato wa ununuzi wa
gari hiyo umegubikwa na utata, kwa madai kuwa fedha ambazo awali
zilitengwa kwa ununuzi wa gari hiyo ni shilingi 84 milioni, wakati
zilizoidhinishwa kwenye bajeti ni shilingi milioni 120.00 tu, hata
hivyo ilionekana ilinunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.
Alisema licha ya ongezeko hilo, lakini pia taarifa haikuonesha fedha za nyongeza zilitoka wapi na kwaidhini ya nani.
Diwani
wa kata ya Lionja, Joachim Mnungu, alisema mkurugenzi alikuwa na kila
sababu ya kuwajulisha madiwani kila hatua iliyohusu mchakato wa ununuzi,
ikiwamo mabadiliko ya mara kwa mara ya bei.
Alisema
fedha zilizokatengwa kwa ajili ya ununuzi ni shilingi 84 milioni. Hata
hivyo kabla ya gari hiyo kuletwa, bei ilipanda na kufikia shilingi 96
milioni.
Kama hiyo haitoshi, baada ya kuletwa waliambiwa imenunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.
"Gari
imekuja na namba za usajili za gari za misaada (DFPA) tena mtumba,
wakala wa manunuzi gani anaweza kuleta gari yenye namba za usajili wa
magari ya misaada," alisema na kuhoji Mnungu.
Mkurugenzi
mtendaji, Mhandisi Masaka akijibu hoja za madiwani hao, alisema ingawa
yeye alikuwa hajahamia katika Halmashauri hii, wakati mambo hayo
yanafanyika.
Lakini
taarifa zinaonesha mchakato ulikwenda sawa bila kukiuka taratibu,
kanuni na sheria. Kwani ununuzi ulifanywa na wakala wa manunuzi wa
serikali(GPSA) na kwamba shilingi 4 milioni ziliongezeka kutokana na
gharama ya kusafirisha gari hiyo ambayo gharama yake halisi ni shilingi
115milioni.
"Hizo
shilingi 95.4 milioni zilirejeshwa na GPSA baada yakuonekana hazitoshi
kununua gari iliyokuwa inatakiwa, ilibidi ziongezwe fedha" gharama ya gari ni shilingi 115, kusafirisha ni dola 4,354 sawa na shilingi 9milioni," alifafanunua Mhandisi Masaka.
Alisema
kiasi kilichongezeka kilitoka kwenye akaunti ya utawala. Nakwamba kiasi
kilichoongezeka(shilingi 4milioni) kiliweza kutolewa bila kupata idhini
ya madiwani kwani sheria inampa mkurugenzi uwezo huo.
Akibainisha
kuwa gari hiyo siyo ya msaada bali walilazimika kuchukua kabla ya
taratibu kukamilika baada ya kupewa maelezo na GPSA kuwa wanaweza
kusubiri hadi taratibu za usajili zikamilike au waipokee na wakati
wowote wakachukue namba za usajili.
"GPSA
walitoa maelekezo kama tunaweza kusubiri au tupokee gari hiyo, ili
baadae ikakachukuliwe baada ya taratibu zote kukamilika ikiwa ni pamoja
na namba za usajili," alibainisha Masaka.
Hatahivyo
majibu hayo hayakuwaridhisha. Diwani wa kata ya Ugawaji, ambaye pia ni
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ahmad Makoroganya, alisema hakubaliani
na majibu hayo kwani hadi baraza la madiwani la Halmashauri hiyo
linavunjwa mwaka jana, mchakato wote kuhusu ununuzi wa gari hiyo ulikuwa
umekamilika, ulibaki ufuatiliaji tu.
Hivyo maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi ilibidi waelezwe kipindi cha mchakato wa ununuzi.
Madai ya madiwani hao yaliungwa mkono na mkuu wa wilaya hii ya Nachingwea, Pololeti Mgema, ambae alisema wataalamu walishindwa kuonesha thamani ya dola kwa shilingi ya Tanzania kwenye mabadiliko hayo ya bei ambayo yalikuwa yanafanyika.
Madai ya madiwani hao yaliungwa mkono na mkuu wa wilaya hii ya Nachingwea, Pololeti Mgema, ambae alisema wataalamu walishindwa kuonesha thamani ya dola kwa shilingi ya Tanzania kwenye mabadiliko hayo ya bei ambayo yalikuwa yanafanyika.
Aliwashauri
madiwani hao waendelee kuhoji ili wapate maelezo yanayojitosheleza
kwenye mkutano au waunde kamati ya uchunguzi, ambayo pamoja namambo
mengine ichunguze uhalali wa gari hiyo kubandikwa namba za usajili wa
magari yanayotolewa kwa msaada na wahisani.
Mvutano ulikwisha baada ya madiwani hao kukubaliana kujadili suala hilo kwenye kikao cha kamati ya madiwani, baada ya baraza hilo kujigeuza nakuwa kamati.
Mvutano ulikwisha baada ya madiwani hao kukubaliana kujadili suala hilo kwenye kikao cha kamati ya madiwani, baada ya baraza hilo kujigeuza nakuwa kamati.
Post a Comment