Hayo yameelezwa na Rais DR. JOHN POMBE MAGUFULI katika hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
DKT HUSEIN MWINYI na pia kuagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha
zinavilinda kikamilifu vyama vya skauti ili visife bila sababu za
msingi.
Rais wa Skauti Tanzania Profesa JOYCE NDALICHAKO ambaye pia ni
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi licha ya
kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi mpya wa skauti
kukiimarisha chama hicho, amesema ni vema chama kikaangalia uwezekano wa
kuongeza wigo wa kuwapata vijana wengi zaidi.
Akitoa maelezo ya utendaji kazi wa chama hicho tangu uanze uongozi
mpya mwaka 2013, Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania ABDULKARIM SHAH
amesema kazi kubwa wanayoifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanarejesha
heshima ya chama hicho iliyokuwa imepotea kwa miaka kadhaa.
Post a Comment