Amesema hatua hiyo ni kuhakikisha kila mtu anatekeleza wajibu wake
wa kulipa kodi ili serikali iweze kutekeleza mipango yake iliyojiwekea
na hivyo amewaomba wananchi kuisaidia serikali kutekeleza oparesheni
hiyo.
Mheshimiwa MAJALIWA ameyasema hayo katika mkutano wa Jumuiya ya
Wanarukwa na Katavi waishio jijini Dar es Salaam ambapo amesema serikali
haitamuonea mtu wala huruma mtu yoyote ambaye anakwenda kinyume na
sheria za nchi.
Aidha mkuu huyo amewataka Watanzania kutumia fursa zinazowazunguka
kama madini, kilimo, mifugo na nyingine za kujiletea maendeleo.
Naye Waziri Mkuu Mstahafu MIZENGO PINDA amesema kwa sasa kila mtu
anapaswa kujua kuwa ni jukumu lake kujiletea maendeleo kwani haitakuwa
na faida yoyote kama mtu amebaki kuikosoa serikali bila ya kutoa njia
mbayala ya kurekebisha hicho ambacho anaona hakijawa sawa.
Post a Comment