Timu ya Manchester United iko mbioni
kuvunja rekodi ya Uingereza kwa kuwa klabu ya kwanza kabisa kuvuna
mapato ya zaidi ya pauni nusu bilioni kwa mwaka mmoja.
Timu hiyo
imezidi kuimarika Kibiashara na wametangaza mapato yao kwa mwaka
yatagonga pauni milioni 500 hadi 510 kitu ambacho hakuna klabu yeyote ya
Uingereza imewahi kufikisha.Mapato kwa robo ya pili ya mwaka yamepanda na kufikia pauni milioni 133.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.6 kutoka ya mwaka uliopita wa fedha.
Mapato kutokana na matangazo yamepanda kwa asilimia 31.3 na yale ya udhamini kwa robo ya pili ya mwaka yamepanda kwa pauni milioni 1.6 na kufikia pauni milioni 37.4.
Pia, Man United sasa wapo kwenye uvumi mkubwa kuwa meneja wao, Louis van Gaal, atabadilishwa mwishoni mwa Msimu na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Post a Comment