Rais Magufuli
Serikali ya
Tanzania imebaini wizi wa takribani shilingi milioni 700 sawa na dola
laki tatu za marekani ($320,000 )katika shirika lake la Ndege (ATCL)
kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel
iliyopo visiwa vya Comoro.
Hii ni moja ya harakati za serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania.Kufuatia upotevu huo wa fedha, mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Steven Kasubi amesimamishwa kazi.
Uchunguzi umeanza chini ya kikosi cha polisi kitengo cha usalama mitandaoni ili kubaini mtandao mzima wa wote walivyohusika.
Post a Comment