Mabao mawili ya Hamisi Kiiza yanaipandisha Simba kileleni mwa ligi
kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa misimu mitatu bila kukaa
kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara na kuacha ligi hiyo ikitawaliwa na
mahasimu wao Yanga, Azam na Mtibwa Sugar ambao wamekuwa wakipokezana
kuongoza ligi hiyo.
Kwa mara ya mwisho Simba iliongoza ligi mwanzoni mwa msimu wa 2013-14 wakati huo Simba ikiwa chini ya kocha Abdalah Kibadeni aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuiongoza Simba kushinda michezo yake mitano ya mwanzo.
Bao la kwanza la Hamisi Kiiza lilitokana na pasi ya Mwinyi Kazimoto ambayo ilimkuta Kiiza aliyeachia shuti kali lililomshinda golikipa wa Stand United Frank Muwonge na kujaa moja kwa moja kambani.
Goli hilo liipa Simba nafasi ya kuongoza 1-0 mpaka dakika za kipindi cha kwanza kinamalizika huku Stand wakiwa hoi.
Kipindi cha pili Simba walipata bao la pili dakika ya 48 ikiwa ni dakika tatu tu tangu kipindi cha pili kuanza baada ya Hassan Kessy kumtoka beki wa kushoto wa Stand United na kuambaa na mpira kisha kutia krosi ambayo ilikwamishwa moja kwa moja wavuni na Hamisi Kiiza ‘Diego’.
Pastory Athanas aliipa Stand United bao la kufutia machozi dakika ya 89 baada ya walinzi wa Simba kujichanganya na kushindwa kuokoa mpira langoni mwao.
Mwelekeo wa ligi
Simba wamerejea kwenye mbio za ubingwa wakitokea nafasi ya nne nyuma ya Mtibwa Sugar na kukwea mpaka nafasi ya kwanza huku wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Yanga lakini wakiwa mbele ya Azam kwa michezo mitatu (3). Simba imecheza michezo 19, Yanga 18 wakati Azam ambao watacheza kesho dhidi ya Coastal Union wakiwa wameshacheza mechi 16.
Rekodi ya Mayanja tangu atue Simba
Jackson Mayanja aliichukua Simba chini ya Dylan Kerr ikiwa nafasi ya tatu ameiongoza kwenye michezo sita ya ligi kuu ya Vodacom na kufanikiwa kushinda michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 18 huku akiwa ameiongoza pia katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Burkina Faso kwenye mchezo wa FA Cup.
Mechi 7 mabao 15
Simba ikiwa chini ya Mayanja imecheza mechi 7 za ligi na kufanikiwa kuweka kambani bao 15 huku ikiruhusu bao 2 tu.
Simba 1-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 0-2 Simba
Simba 4-0 African Sports
Simba 5-1 Mgambo JKT
Kagera Sugar 0-1 Simba
Stand United 1-2 Simba
Kuelekea Kariakoo Derby (Yanga vs Simba)
February 20 Simba wataingia kwenye mchezo dhidi ya Yanga wakiwa na morali ya juu baada ya kushinda michezo yao sita kabla ya pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wao huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Hamisi Kiiza na mbio za ufungaji bora
Kiiza amefunga magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Stand United na kufikisha jumla ya magoli 16 hadi sasa akiwa anaongoza kwenye orodha wafungaji bora kwenye msimu huu.
Amis Tambwe ndiyo anamfati Kiiza akiwa na magoli 14 huku Jeremia Juma Mgunda (Tanzania Prisons) na Kipre Tchetche (Azam FC) kila mmoja.

Post a Comment