Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena leo
February 13 kwa jumla ya michezo 7 kupigwa katika viwanja kadhaa
Uingereza, Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo ambayo msimu huu wamekuwa
wakisuasua kupata matokeo mazuri, klabu ya Chelsea The Blues walikuwa
wenyeji wa Newcastle United katika dimba la Stamford Bridge.
Klabu ya Chelsea ambayo bado ipo chini
ya kocha wa muda Guus Hiddink imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa
jumla ya goli 5-1 dhidi ya Newcastle United, ushindi ambao umewafanya
wafikishe jumla ya point 33, wakiwa nafasi ya 12 katika michezo yao 26
waliocheza katika Ligi Kuu msimu huu, ushindi huo umekuja wakati ambao
Chelsea ilidumu kwa nafasi ya 13 kwa wiki kadhaa.
Magoli ya Chelsea yalianza kufungwa dakika ya 5 na Diego Costa, Pedro Rodriguez dakika ya 9, Willian dakika ya 17, Pedro
Rodriguez tena dakika ya 59 na Bertrand Traore akapiga goli la tano
dakika ya 83, Newcastle United walipata goli la kufutia machozi dakika
ya 90 kupitia kwa Andros Townsend. hivyo mchezo ulimalizika kwa Chelsea
kuibuka na ushindi wa goli 5-1, huku Newcastle United ikibaki kushika
nafasi ya 18 kwa point 24 katika michezo yao 26 ya Ligi.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa February 13
Post a Comment