0
 Mzozo
Rais Magufuli ameshauri wasiokubaliana na hali waende mahakamani
Rais John Magufuli amesema hataingilia mzozo wa kisiasa ambao unaendelea visiwani Zanzibar kuhusu uchaguzi.
Akiongea na Wazee wa Dar es Salaam, katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja katika vyombo vya habari, Dkt Magufuli amesema hakusudii kamwe kuingilia mzozo huo.
“Kuhusu Zanzibar, kama tume za uchaguzi nyingi duniani, haiwezi kuingiliwa na Rais yeyote ndiyo maana tume za uchaguzi huwa huru,” amesema Dkt Magufuli.
“Napenda kuheshimu sheria. Hiyo ZEC ina uhuru wa kuamua mambo yake lakini kama kuna tafsiri mbaya, waende mahakamani, mahakama ziko pale halafu unamwambia Magufuli ingilia.
Jukumu langu kama amiri jeshi mkuu ni kuhakikisha amani ya Zanzibar inaimarika, yeyote atakaeleta fyokofyko ajue vyombo vya usalama vipo."
Chama cha Wananchi (CUF) mwezi uliopita kilikuwa kimetoa wito kwa kiongozi huyo wa jamhuri ya muungano kuingilia kati.
Mzozo visiwani humo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 20 Oktoba mwaka jana.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza kwamba uchaguzi utarudiwa 20 Machi, hatua iliyopigwa na viongozi wa CUF ambao wamesema watasusia.

Post a Comment

 
Top