Msimamo huo wa serikali umetolewa na naibu waziri wa muungano na
mazingira wa serikali ya muungano mhe luhanga mpina baada ya kutembelea
maeneo yaliyukubwa na uharibifu huo katika eneo la Kilimani Zanzibar
ambapo aliweza kushudia maji ya bahari yanavyotafuta ardhi na
kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ambapo naibu waziri amesema
fedha zipo na kutaka upandaji na uwekaji wa matuta unaanza mara moja.
Mapema mkurugenzi wa mazingira wa Zanzibar Juma Bakari Alawai
amesema mabadiliko ya tabia nchi yahatarisha eneo hilo na endapo hatua
za haraka hazita chukuliwa eneo hilo lote litageuka bahari na
kuhatarisha maisha ya wananchi na maendeleo ya nchi.
Naibu waziri Mpina anakuwa waziri wa kwanza anayeshugulikia masuala
ya muungnao kufika Zanzibar na kungalia kero na matatizo ya wananchi na
kutekeleza hatua hizo kwa vitendo na kutoa ahadi za uhakika.
Post a Comment