Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde.
Kwenye mitihani ya taifa iliyopita, baadhi ya wanafunzi walikuwa
wakiandika mashairi ya nyimbo za muziki wa kizazi kipya kwenye karatasi
za majibu na wengine kuchora vitu mbalimbali ikiwa pamoja na mfano wa
picha ya mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi, na picha nyingine za
kutisha maarufu kama ‘zombie’.
Dk. Msondo aliiamba Nipashe kuwa: “Watahiniwa wamejibu kadri ya
uwezo wao ulivyowatuma. Kwa mwaka huu hatujabaini watu ambao wameandika,
mazombi wala freemason.
"Tunachokiona ni kwamba watahiniwa walioshindwa wanaandika majibu
ambayo hayana uhusiano kabisa na baadhi ya maswali waliyoulizwa. Hawa
ndio wengi wamepata sifuri na wengine alama za chini kabisa,” alisema
Dk. Msonde na kuongeza:
“Ukiangalia watahiniwa waliofanya mitihani mwaka huu ni wengi
kidogo. Wako 433,633 ukipata watu kama 20 wameandika hayo mambo
yasiyoeleweka kwa kweli si idadi ya kutisha.
"Tunachofurahi ni kwamba walijibu. Ile ni hatua moja, wanajibu,
wanaandika, hata kama majibu hayaelezi kile kilichotakiwa ni faraja,
unapata picha kwamba hawa watu wamekosa maarifa, stadi na uelewa wa mada
zile. Wamejibu kama walivyopata majibu kwa wakati huo.”
Alisema kazi wanayofanya kwa sasa ni uchambuzi wa kina wa matokeo
ili wajue ufaulu kwa kila mada, kila mtahiniwa na kila swali ulikuwaje
na baada ya hapo watatoa machapisho ya kupeleka kwa walimu.
Akijibu juu ya ufaulu wa hesabu kuendelea kuwa wa chini, alisema wanachokiona ndiyo kitu kinachoendelea darasani.
“Kwa huu ufaulu hata ukisema ule wa mwaka 2014 wa asilimia 19.58
na asilimia 16.76 ya mwaka huu (2015), tafsiri yake inakwambia kwamba
tunao watahiniwa zaidi ya asilimia 80 ambao wanashindwa somo hili. Hali
hii si nzuri.
"Tukiangalia Historia ni kwamba ufaulu wa hesabu kwa miaka mingi
umekuwa chini. Hii inaonyesha darasani kuna kitu kinachotakiwa kufanyiwa
kazi. Ukiona ufaulu uko chini au uko juu, ni kiashiria kinachojiri
darasani. Kupanda au kushuka kwa ufaulu ni kiashiria ya kile mwalimu
anachofanya darasani, uongozi wa shule, wazazi, walimu, wanafunzi, mkoa
wilaya wanavyoshirikiana.”
"Je, walimu wana ari? Wapo wa kutosha? Wana maarifa, wanatekeleza
majuku yao kikamilifu? Wanahamasisha vijana? Au wanakatisha tamaa?
Watoto wana utayari wa kujifunza? Kama walimu na wanafunzi wako vizuri,
uongozi wa shule? mkuu wa shule, kamati za shule, wazazi, wanashirikina
vizuri?” alihoji Dk. Msonde
Akizungumza matokeo ya mwaka huu kushuka kidogo ilhali tangu 2013
yalikuwa yakiongezeka, Dk. Msonde alisema: “Sisi kitaalamu kushuka kwa
asilimia 0.8 si kushuka. Ingawa bado sisi kama baraza ni vigumu kusema
kwa nini umeshuka kidogo, ila kwa haraka haraka ni idadi ya watahiniwa,
433,633 waliofanya mtihani mwaka 2015, ukilinganisha na mwaka 2014 ambao
walikuwa 288,247, hivyo kwa haraka kuna kundi la zaidi ya 150,000
limekuja hapa.”
Alisema kwa kawaida watahiniwa wa kidato cha nne hawajawahi kuwa
200,000 lakini kwa sababu wengi walipunguzwa 2012, walioweza kufanya
mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 walikuwa wachache.
“Kitendo cha watahiniwa zaidi ya 400,000 na matokeo yakabaki
palepale, nasema ufaulu umeimarika, ndiyo maana ukisema ubora wa ufaulu
daraja la kwanza mpaka la tatu, bado watakuwa ni wengi kuliko mwaka
jana.
Post a Comment