Serikali ya Somalia
imelalamikia vikali hatua ya maafisa wa usafiri wa ndege nchini Kenya
kuwanyima ruhusa ujumbe ulioandamana na waziri mkuu wa Somalia ruhusa
ya kuabiri ndege ya kwenda Uturuki.
- Mwishoni mwa juma ndege iliyokuwa imembeba waziri mkuu Abdirashid Sharmarke na wajumbe wake ilizuiliwa kwa muda kutokana na wajumbe kadhaa kukosa ruhusa ya kuingia Kenya.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Somalia inaitaka Kenya, ielezee waziwazi kwanini hilo lilitokea ilihali kunamakubaliano rasmi kati ya serikali hizo mbili kuhusiana na usafiri wa maafisa wakuu serikalini.
Waziri mkuu hata hivyo amekiri kuwa hakuzuiliwa na kuwa waliozuiliwa ni wajumbe walioambatana naye.
Post a Comment