0

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuwawa kwa wanyama zikiwemo mbuzi zaidi ya 70.  
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti),wakiwemo na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuuwawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Dihinda mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi  na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi  kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

February 9 2016 waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba alilazimika kusafiri haraka hadi mkoani Morogoro kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero, baada ya taarifa za mapigano ya wakulima na wafugaji kumfikia, safari hii yameingia kwenye headlines nyingine ya kuuwawa zaidi ya mifugo 75 kati ya mifugo 200 waliojeruhiwa kwa mapanga.
IMG-20160209-WA0019
Waziri Mwigulu amefika eneo la tukio na kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza kamati ya ulinzi ya mkoa na wilaya, kufanya uchunguzi na kuwatafuta wahusika wa tukio la kukatwa katwa mapanga kwa zaidi ya mifugo 75, ili wafike mbele ya mikono ya sheria nakuagiza mahakama kupitia upya hukumu iliyotolewa mwaka 2015 ya kugawa mipaka kati ya eneo la wakulima na wafugaji.
IMG-20160209-WA0018
Mwisho waziri Nchemba ameagiza uongozi wa mkoa na wilaya kufanya mkutano wa hadhara wa wakulima na wafugaji tarehe 20/02/2016, ili kuanza  harakati za kumaliza mgogoro. Kati ya mifugo inayotajwa ni mbuzi, kondoo na ndama.
IMG-20160209-WA0017
IMG-20160209-WA0016
IMG-20160209-WA0015
IMG-20160209-WA0025
IMG-20160209-WA0024
IMG-20160209-WA0013
IMG-20160209-WA0022
IMG-20160209-WA0021
IMG-20160209-WA0020

Post a Comment

 
Top