![]() | |
|
POLISI
mkoani Simiyu imewatia mbaroni watu tisa, wanaotuhumiwa kuwa ni
majangili waliohusika na kifo cha rubani Mwingereza katika Pori la Akiba
la Maswa, huku ikikamata bunduki 29 na meno ya tembo matatu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Lazaro Mambosasa alisema wamewakamata
watuhumiwa tisa wa tukio la kuangusha helikopta pamoja na kusababisha
kifo cha rubani wa ndege hiyo, Kapteni Gower Roger (24) ambaye mwili
wake ulisafirishwa wiki iliyopita kwenda kwao kwa maziko.
Kamanda
Mambosasa alisema walifanya msako mkali, uliowezesha kukamatwa
watuhumiwa wawili ambao ni Shija Mjika (38) na Masasi Mandogo (48),
waliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wengine saba wa tukio hilo.
Alisema
baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili, walitaja na kuonesha meno
mawili ya tembo yenye kilo 31 aliyeuawa Januari 29, mwaka huu ambayo
walikuwa wameyaficha kwenye daraja katika kijiji cha Itaba.
Alibainisha
kuwa baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Polisi iliwahoji na kukiri
kuhusika na tukio hilo na kumtaja ambaye alifyatua risasi kwenye
helikopta, ambaye ni Dotto Pangali (41) ambaye alikamatwa akitaka
kujaribu kutoroka kwenda mkoani Shinyanga.
Kamanda
Mambosasa alisema baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, alikiri
kutungua helikopta hiyo kwa kutumia bunduki ya Riffle yenye namba
7209460 CAR NA 63229 inayomilikiwa na Mange Balum ambaye kwa sasa
anashikiliwa na Polisi.
Alisema
baada ya upekuzi wa kina kwenye mji wa Pangali, kulipatikana bunduki
aina ya Riffle yenye namba 3478 CAR Na 458 ikiwa na risasi sita,
inayomilikiwa na Nghomango Jilala aliyekimbia na anaendelea kutafutwa.
Alifafanua
kuwa katika operesheni hiyo pia waliwakamata watuhumiwa wengine ambao
ni Njile Gonga (28), Iddi Mashaka (49), Mwigulu Kanga (40), Mapolu Njige
(50) wote wakazi wa kijiji cha Sungu, Dotto Huya (45) mkazi wa kijiji
cha Itaba pamoja na Mange Balum (47) pia mkazi wa Itaba wilayani Meatu.
“Katika
msako huo tumefanikiwa kukamata bunduki 27 pamoja na risasi 141 ambazo
zina wamiliki, ambao wamekuwa wakizikodisha silaha hizo kwa majangili
kwenda kuulia tembo katika hifadhi za taifa na tumekamata Shot gun 11 na
risasi 44, Riffle 10 na risasi zake 105 pamoja na magobole sita yakiwa
na risasi mbili,” alisema Kamanda.

Post a Comment