RAIS
John Magufuli amesema hatua ya kurudia uchaguzi Zanzibar ndio njia
sahihi ya kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani humo. Rais Magufuli
aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya aliyowaandalia
mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao Ikulu, Dar es Salaam.
Dk
Magufuli aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga aliyesoma
hotuba kwa niaba yake. Alisema kufanyika uchaguzi wa marudio kutasaidia
kuondoa mvutano wa kisiasa uliopo na kusisitiza kuwa mazungumzo kati ya
vyama vya siasa yaliyoanza Novemba mwaka jana, hayakufikia mwafaka wa
namna ya kutatua tatizo hilo.
“Zanzibar
ina mfumo wake wa siasa, ina Katiba na ina Tume huru ya Uchaguzi. Hatua
ya kufanya uchaguzi ndio njia sahihi katika hali ya sasa katika
kumaliza tatizo hilo. “Chama kikuu cha upinzani (CFU) wanadai
wameshinda, lakini chama tawala na vyama vingine vinaona haja ya kufanya
uchaguzi wa marudio ili kuondoa kasoro,” alisema Dk Magufuli.
Alisema
mlango wa mazungumzo juu ya namna ya kufanya uchaguzi wa marudio kuwa
huru na haki na kufuata taratibu za kimataifa uko wazi na kuwa ni imani
yake nchi marafiki wa Zanzibar na Tanzania wataunga mkono juhudi hizo.
“Kama
ilivyo kwa Watanzania wengi wanavyoona, njia ya kuthibitisha ushindi ni
boksi la kura na kukataa kushiriki ni kukataa kufikia mwafaka na
serikali na kujinyima haki ya miaka mitano ijayo,” alisema Rais.
Aidha,
alisema bado kuna siku 40 ambazo zinatosha kuwa na mazungumzo ya kuja
na suluhisho la tatizo hilo. Zanzibar inatarajia kufanya uchaguzi wa
marudio Machi 20, mwaka huu kutokana na uliofanyika Oktoba 25, mwaka
jana kufutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Mbali
ya suala la Zanzibar, Rais Magufuli alizungumzia mambo mengine ikiwamo
rushwa, umasikini na ukosefu wa ajira, na kuwaeleza mabalozi hao kwamba
nia ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati mwaka
2025 haitafikiwa kama changamoto hizo hazitaondolewa.
|
Post a Comment