Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena hapo kesho kwa jumla ya michezo sita kuchezwa.
Macho
na masikio ya wapenda soka yatakua yakisubiri kwa hamu Dabi ya kariakoo
kati ya Wekundu wa msimbazi Simba Sport Klabu, dhidi ya timu ya
wananchi Dar Young Afrikans Yanga, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la
taifa Jijini Dar Es Salaam.Michezo mingine itayaopigwa hapo kesho Mgambo Jkt wataonyeshana ubavu na Tanzania Prisons, Stand United wao watawalika Jkt Ruvu.
Mbeya City wao watakua nyumbani Sokoine kukupiga na Wanalambalamba Azam FC , huku wanalizombe Majimaji wakikipiga na wakata miwa wa Mtibwa Sugar .Toto Africans ya Mwanza, wao watawalika jirani zao kutoka mkoani Kagera, Kagera Sugar.
Post a Comment