Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai
(CHADEMA) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na
Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.
Akitangaza
Mawaziri hao vivuli kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani amesema
anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote
walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani ili kupeleka
mbele gurudumu la maendeleo nchini.
Waliotangazwa
Katika Orodha hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora Jaffar Michael, Manaibu wake ni Joseph Nkundi
na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Ali Saleh Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Esther Bulaya na
Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi ina mawaziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Inj. James Mbatia na Naibu
Waziri Willy Kombucha.
Aidha
ameendelea kuwataja Mawaziri wengine kuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango
Halima Mdee na Naibu Waziri ni David Silinde, Waziri wa Nishati na
Madini John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri wa Katiba na
Sheria Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya
Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa
na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya
Ndani Godbless Lema na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
Naibu Waziri Salum Mgoso.
Wengine
walioteuliwa katika Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii
Esther Matiko na Naibu Waziri Cecilia Pareso, Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Anthony Komu na Naibu Waziri Cecil Mwambe, Waziri
wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Suzan Lyimo Naibu Waziri Dkt. Ali
Suleiman Yusuph, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri
Devotha Minja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Hamidu Hassan na Naibu
Waziri Peter Lijualikali.

Post a Comment