0
Uganda: Museveni ashiriki mjadala wa runinga
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa akitetea rekodi yake ya kisiasa katika hotuba ya kwanza kabisa ya runinga.
Wagombezi wote saba wa upinzani walihudhuria mjadala huo wa umma, uliofanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili mjini Kampala, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu hapo Alhamisi ya wiki hii.
Huku mamilioni ya raia wa Uganda wakifuatilia mjadala huo, Bwana Museveni alisema kuwa madai ya wapinzani wake dhidi ya ufisadi serikalini ni dhana tu.
Rais Museveni , 71, anatafuta uungwaji mkono katika azimio lake la kuendeleza utawala wake wa miaka 30.
Museveni atakuwa anawania muula wake wa 5.
Mada kuu usiku wa jana katika mjadala huo wa wawaniaji kiti cha urais nchini Uganda ilikuwa sera za kigeni,na usalama wa taifa.
Mdahalo wa kwanza kama huo uliofanyika majuma kadhaa yaliyopita yaliangazia maswala ya kitaifa huduma ya afya ya umma na elimu.
 
Uchaguzi mkuu wa Uganda umeratibiwa kufanyika hapo Alhamisi ya wiki hii.
Museveni hakuhudhuria mdahalo huo akidai kuwa ulikuwa ni mdahalo wa kitoto.
Wachanganuzi wa maswala ya siasa wanasema kuwa Museveni alikuwa mtuliwa kuliko kawaida yake.
Aidha aliposhiriki mjadala alitoa kauli zake kwa uwazi wala hakutapatapa wala kuchachawizwa na wapinzani wake.
Wagombea nane watashiriki katika uchaguzi huo mkuu.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Museveni kukabiliwa na upinzani mkali.
 
Wagombea nane watashiriki katika uchaguzi huo mkuu wa urais.
Museveni ambaye anaiwakilisha dola tawala ya National Resistance Movement NRM anatarajia upimnzani mkali utoka kwa Kizza Besigye, na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.
Kanali Kizza Besigye, ni mwakilishi wa chama cha upinzani Forum for Democratic Changehuku waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi, akiwa mgombea huru.
Hata hivyo Mbambazi anaungwa mkono na vuguvugu la GoForward .

Post a Comment

 
Top