0

Makamu wa pili wa rais wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu kuacha kudanganyana na badala yake wasubiri muda utakapofika rais atakaye tangazwa ataapishwa na kuchukua madaraka ya kuiyongoza Zanzibar.
Balozi Seif ameyasema hayo hapa Kianga Ole mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara mpya kutoka Ole hadi Kengeja yenye urefu wa kilo mita 35 ikiwa nimiongoni mwa shamrashamra ya madhimisho ya mika 52 ya mapinduzi ya Zanzibar zinazoendelea Unguja na Pemba.
 
Aidha balozi Seif amesema nivyema kwa wafanyakazi kila moja kwa nafasi yake kuwajibika kuhakikisha hawachii watu kujenga karibu na barabara kwani sio busara kumvunjia mtu aliejenga watendaji wapo nakumwachia kisha kumvunjia nyumba yake badala yake azuiwe wakati anataka kujenga.
 
Mapema katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na miundombino wa serekali ya Mapinduzi Zanzibar Juma Maliki Akili amesema zaidi ya  dola milioni 12 zitatumika katika ujenzi wa barabara hiyo ambapo dola milioni moja zitatolewa na serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwaajili ya kulipa fidia kwa wananchi na zilizo bakia ni msada kutoka shirika la mafuta ulimwenguni OPEQ.
 
Nae mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Bi. Mwanajuma Majidi Abdalla amesema kumalizika kwa barabara hio nikiunganishi muhimu kati ya mkoa wa kusini na kaskazini Pemba.
 
Ujenzi wa barabara hio ya Ole Kengeja ulianza  01.09.2014 hadi sasa imefikia kilomter 11 tu kwakiwango cha kifusi  inatarajia kutumia miezi 36 ya ujenzi wabarara hio tayari imekwisha tumia miezi 16 bado miezi 20 tu ambayo itajenga.

Post a Comment

 
Top