0
 
Henriette Reker meya wa mji wa Colgne
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake wapatao tisini walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.
Polisi pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la cathedral, ambalo lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa Ki arab ama Afrika Kaskazini.

Merkel ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kugundua ukweli kuhusiana na madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika ,bila kujali asili yao ama historia za awali.

Meya wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu hatua zitakazochukuliwa zitende haki bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani.Na akachukua hatua ya kufanya mazungumzo ya dharula na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo; ambapo Polisi waliahidi kuimarisha ulinzi.BBC

Post a Comment

 
Top