0
  
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi Hassan Masala.

Christopher Lilai,Nachingwea.
   Mbunge wa jimbo la Nachingwea,Hasani Masala ametoa pikipiki tatu zenye thamani ya shilingi milioni sita na fedha taslimu  shilingi laki tano kwa Umoja wa madereva wa bodaboda wilayani hapa huku akiwataka kusajili umoja huo ili utambulike kisheria.

    Mchango huo ameutoa alipokutana na madereva wa bodaboda siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Nachingwea Resort ambapo licha ya kusikiliza kero mbalimbali wanazokutananazo aliwahasa kuunda umoja wenye nguvu na kuwa na mfuko wa kuweka na kukopa ili uwasaidie katika kuwapatia mitaji.

   Aliwataka viongozi wa umoja huo kuwatambua madereva wote wa bodaboda wilayani na kwa kupitia vituo vyao vya kazi maarufu migundi kuunda uongozi ambao ndio utakuwa ndio wawakilishi wa kila mgundi hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya uongozi na taasisi mbalimbali ikiwemo jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.

   Masala alisema kuwa msaada wa pikipiki alizowapatia ni mtaji katika  kuanzisha VICCOBA endelevu ambapo ndio patakuwa kimbilio kwa madereva hao ili kuachana na kutumwa na badala yake waweze kumiliki pikipiki zao wenyewe kwa kukopeshana wenyewe kupitia mfuko huo.

    “Mimi nipo nyuma yenu katika kuhakikisha mnafanikiwa kuunda  mfuko wa Viccoba endelevu ambacho ndicho chombo pekee kitakachokuwa mkombozi wenualisema Masala.

     Aliwahasa madereva hao wa bodaboda kuacha kutumiwa vibaya na wanasiasa kwani muda wa siasa umepita badala yake waendelee na majukumu yao ya kujitafutia kipato na serikali ipo nyuma yao na iwapo kuna tatizo ofisi yake ipo wazi kupokea malalamiko yao.
r

Post a Comment

 
Top