Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akumjulia hali mtoto Jack Issac aliyelazwa kwa matibabu katika
hospitali ya Mkoa wa Geita leo Januari 05, 2016 wakati alipofika
hospitalini hapo kwa ajili ya kukagua hali za wagonjwa na kukabidhi
Vifaa mbalimbali vya tiba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikabidhi kifaa cha Tiba kwa mganga Mkuu wa Hospitali ya Geita Dkt.
Joseph Kisala wakati alipofika hospitalini hapo kwa leo Januari 05, 2016
kwa ajili ya kukagua hali za wagonjwa na kukabidhi Vifaa vya tiba,
Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo
ya wananchi, kulshoto ni waziri wa Afya Mhe. Ummi Mwalimu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikabidhi Tunzo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa
madini GGM Terry Melpeter kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na
kampuni yake katika kusaidia maendeleo Mkoani Geita, Makamu wa Rais yupo
Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa Geita
uliofadhiliwa na kampuni ya Uchimbaji madini ya GGM Mkoani humo leo
Januari 05,2016, Makamu wa Rais yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimtwisha Ndoo ya maji Bibi Veronika Lupanjo baada ya kuzindua mradi wa
maji safi na salama Mkoani Geita leo Januari 05,2016. Makamu wa Rais
yupo Mkoani Geita kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi.
Post a Comment