0

Ufaransa
Mamia ya misikiti nchini Ufaransa imefunguliwa wageni katika juhudi za kuanzisha mazungumzo ili kuondoa dhana potofu kuhusu Waislamu na Uislamu.
Raia wamekaribishwa kunywa chai na kufanya mijadala pamoja na sala.
Mpango huon unajiri mwaka mmoja baada ya wapiganaji wa Islamic State kushambulia gazeti la Cherlie Hebdo pamoja na duka la jumla la wayahudi mjini Paris.
Mkuu wa shirika la waislamu nchini Ufaransa Anouar Kbibech wa baraza la Waislamu amesema kuwa mkusanyiko huo unalenga umoja ulioonyeshwa wakati wa shambulizi hilo ili kusaidia kuimarisha utangamano wa kitaifa.

Post a Comment

 
Top